DEGEDEGE.
DEGEDEGE. Degedege ni nini? Ni hali inayotokea kwa kukaza na kuachia kwa misuli mbalimbali ya mwili bila utaratibu maalumu na kupelekea mwili kuwa na mijongeo isiyokuwa ya kawaida. Hali hii husababishwa na utolewaji mbaya wa chaji katika seli za mfumo wa fahamu ndani ya Ubongo, Tatizo hili linaweza kuwapata watu wazima au watoto. Lakini mara nyingi zaidi hutokea kwa watoto. VISABABISHI VYA DEGEDEGE. A. MAGONJWA MBALI MBALI I. Homa ya uti wa mgongo. (Meningitis) II. Homa kali ya malaria/Malaria Sugu (Malaria) III. Maambukizi ya bakteria kwenye damu{mchafuko wa damu} (septicaemia) ...