DEGEDEGE.

DEGEDEGE.
















Degedege ni nini?

 Ni hali inayotokea kwa  kukaza na kuachia kwa misuli mbalimbali ya mwili bila utaratibu maalumu na kupelekea mwili kuwa na mijongeo isiyokuwa ya kawaida.

 Hali hii husababishwa na utolewaji mbaya wa chaji katika seli za mfumo wa fahamu ndani ya Ubongo,

Tatizo hili linaweza kuwapata watu wazima au watoto. Lakini mara nyingi zaidi hutokea kwa watoto.

VISABABISHI VYA DEGEDEGE.

A.      MAGONJWA MBALI MBALI
I.                    Homa ya uti wa mgongo. (Meningitis)
II.                  Homa kali ya malaria/Malaria Sugu (Malaria)
III.                Maambukizi ya bakteria kwenye damu{mchafuko wa damu} (septicaemia)

B.       HALI ZA KIUTENDAJI ZA MWILI
I.                    Kushuka kwa kiwango cha sukari mwilini (Hypoglycaemia)
II.                  Kupungua kwa kiwango cha Sodium mwilini (Hyponatremia)
III.                Kupungua kwa kiwango cha Magnesium mwilini (Hypomagnesaemia)

C.      MAJERAHA
Mtu anapoapata majeraha kichwani anaweza kupata hali ya degedege.


D.      KUSHUKA KIWANGO CHA HEWA YA OKSIJENI MWILINI.
Kwa mtoto mchanga aliyechelewa kutoka wakati wa kujifungua anaweza kupatwa na hali ya kuwa na kiwango kidogo cha hewa ya oksijeni  iitwayo (Birth asphyxia) na ikamsababisia kupata Degedege.


E.       MATATIZO MBALI MBALI KWENYE UBONGO.
I.                    Kuvia damu ndani ya ubongo
II.                  Vimbe mbali mbali
III.                Usaha
IV.                Minyoo (Cyssticecosis)

F.        SUMU MBALI MBALI
I.          Alcohol consumption
II.       sumu za madini ya lead  na Mekyuri
III.    Sumu za caboni-monoksaidi

G.     KIFAFA.
Kifafa ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu kwenye ubongo hivyo kusabaisha degedege.

Hizi ni baadhi tu ya sababu za Degedege, na zinaweza kutibika pale utakampompeleka Mgonjwa katika kituo cha hudama ya afya haraka iwezekanavyo. 

Angalizo:
 usitumie dawa bila mgonjwa wako kuonwa na daktari kwani degedege ni dalili ya magonjwa mengi sana hivyo ni vyema anonwe na wataalamu wampe matibabu husika, na kutibu chanzo cha tatizo.

Tukutane kwenye makala nyingine.

Ahsante.

Kwa maswali/tiba/maelezo zaidi
Whatsapp +255763832798.

Comments