KUPOTEZA HAMU YA KULA KWA WATOTO
Kupoteza hamu ya kula
kwa watoto: Sababu za kupoteza hamu ya kula na Jinsi ya kukinga tatizo hili.
· Sababu za kupoteza hamu ya kula kwa watoto:
· Jinsi ya kukinga kupoteza hamu ya kula kwa watoto:
· Jinsi
ya kuongeza hamu ya chakula kwa watoto.
· Virutubisho
vya kusisimua hamu ya kula.
Sababu za kupoteza hamu ya kula kwa watoto
1. kupungua kwa kasi ya ukuaji:
Mabadiliko ya ukuaji wa mtoto
yanaweza kusababisha kupoteza hamu ya kula kwa mtoto. Kipindi cha mwaka wa
kwanza, mtoto hukua kwa kasi sana, lakini baada ya hapo kasi ya ukuaji
hupungua, na mtoto anaweza kuanza kula kidogo. Katika kipindi hiki kupungua kwa
hamu ya kula kwa mtoto ni kawaida.
2. Maradhi:
Maradhi mara nyingi yanasababisha
kwa kiasi kikubwa kupoteza hamu ya kula kwa watoto, kama mtoto anaumwa,
tonsils, mafua, tumbo, kuharisha, kichwa, homa, na dalili nyinginezo, atakuwa
anakula kidogo kuliko anavyopaswa kula, kwa bahati nzuri watoto wengi hamu ya
kula hurejea wanapopata nafuu.
3. Msongo wa mawazo:
Inaweza kuonekana
kuwa ni kitu kigeni/cha kushangaza lakini msongo wa mawazo ni hali ambayo
inaweza kumpata mtoto pia, na ikamletea matatizo mengi ikiwemo na kupoteza hamu
ya kula. Ukiona mtoto anapoteza hamu ya kula na anapata shida kulala, anaweza
kuwa na msongo wa mawazo. Ili kumsaidia kuondokana na tatizo la kupeteza hamu
ya kula kwa sababu ya msongo wa mawazo unapaswa kugundua sababu za msongo wa
mawazo kwa watoto.
Baadhi ya
sababu hizo ni:
·
Changamoto za familia kama msiba,
kifo cha mnyama aliyepenwa na mtoto, kuzaliwa mtoto mwingine n.k
·
kuonewa
·
kushindwa kuendana na hali ya
masomo.
·
Kuzuiliwa kufanya vitu anavyovipenda
6. Madawa:
Ikiwa
mtoto amekuwa kwenye matumizi ya madawa mbalimbali hususani dawa za kuua
backteria(antibaiotiki), hamu yake ya kula itapungua, kupoteza hamu ya kula kwa
watoto hutokea kama maudhi madogo ya dawa mbalimbali.
7. Upungufu wa Damu:
Upungufu wa
damu ni sababu pia ya mtoto kupoteza hamu ya kula, mtoto anayepitia changamoto
hii, ataonekana mchovu sana, na mdhaifu sana, pia anakuwa msumbufu kwa wengine.
Asipotibiwa tatizo hili atakuwa na ukuaji mbaya na atashindwa kufanya vizuri
shuleni. Mpeleke mtoto apimwe damu kama utahisi ana upungufu wa damu.
8. Minyoo ya Tumboni:
Minyoo ya tumboni inaweza kumpotezea
hamu ya kula mwanao. Minyoo huingia ndani ya mfumo wa chakula wa mtoto wako na
kuishi humo kama tegemezi, wakisababisha kuvuja damu kwenye utumbo, kupoteza
hamu ya kula, kuharisha damu n.k.
9. Kutopata Choo kubwa:
Kama utumbo
wa mtoto hautakuwa katika mijongeo mizuri, mtoto hatapata choo, kupoteza hamu
ya kula ni dalili halisi ya Kukosa Haja kubwa.
Kukosa
hamu kwa mtoto kunaepukika kwa urahisi kwa kufuata mbinu zifuatazo..
Jinsi ya kukinga kupoteza hamu ya kula kwa watoto:
·
Fanya vyakula viwe na muonekana wa
kuvutia kwa mtoto. Kwa mfano: unaweza kupakua chakula kwenye sahani yenye umbo
la kitu anachopenda mtoto, labda sahani yenye umbo la Gari/picha za magari n.k
·
Usibishane na mwanao au kumsema sema
inapofika muda wa kula.
·
Rekebisha ratiba ya chakula, umpe
mtoto chakula wakati ana njaa.
·
Mtie moyo mtoto kuchagua vyakula
vinavyoleta afya.
·
Mruhusu kula kidogo kidogo, kwa
nyakati tofauti tofauti.
·
Usimlazimishe mtoto kula kama hana
njaa.
·
Usimlazimishe amalize chakula chote
kwenye sahani yake, hili sio wazo zuri kwake.
Nyongeza juu ya hapo hizi ni njia za
kuongeza hamu ya chakula kwa watoto.
Jinsi ya kuongeza hamu ya chakula kwa watoto.
Hizi ni njia za kuboresha hamu ya
kula ya mtoto wako, hizi ni njia za kawaida za nyumbani. Lakini pia nimekuwekea
bidhaa bora inayosaidia kwa haraka kuboresha hamu ya kula kuanzia watoto hadi
watu wazima.
·
Watoto wanapenda kula vitu vidogo
vidogo. Lakini hivi vyakula vidogo vidogo vinapaswa viwe bora kama mlo kabisa. Kwa
mfano, mpe mtoto karanga za kukaangwa/korosho badala ya biskuti/crisps.n.k
Karanga zinafahamika kwa uwezo
mkubwa wa kuongeza hamu ya kula na kujenga mwili kwa sababu ya kuwa protini. Hata
vyakula vyake pendelea kuweka karanga.
·
Mruhusu kucheza/ kujihusisha na
mazoezi, hii itamsaidia kupata hamu ya kula vizuri, kuendesha baiskeli,
kujihusisha na michezo mbali mbali ni njia bora za kumfanya mtoto awe na hamu
ya kula.
·
Kama mtoto amepunguza hamu ya kula
mpe chakula kidogo kidogo hadi atakapoanza kula vizuri yeye mwenyewe. Kiasi kidogo
cha chakula kitaongeza mmeng`enyo wa chakula na baadae kuongeza hamu ya kula.
·
Mpe chakula chenye kalori nyingi,
hii itamsaidia hata akila kidogo tayari atakuwa amepata chakula cha kumsaidia
mahitaji ya mwili wake na kuongeza uzito.
·
Mpe maji ya kunywa dakika 30 kabla
muda wa kula chakula.
Pia kumbuka….
·
Tumia viungo mbali mbali vya
kuongeza ladha ya chakula, hivi vinapatikana kwa urahisi sokoni.
·
Limao, tangawizi, and vinega vinasisimua
na kuongeza hamu ya kula.
·
Changanya mboga mboga za rangi
tofauti ili ziwe za kuvutia, kwa mtoto wako.
·
Mtengenezee vinywaji vizito (smoothie)
kwa kutumia zabibu, asali na maziwa ya mgando.
Kwa maelezo zaidi/maswali na tiba nk.
wasiliana na
Dr. James Makala
jamesmakala40@gamil.com
Phone/ whatsapp 0763832798.
Good, very powerful and successful idea, GOD strengthen you in advance.
ReplyDeleteI like it fully.
You are welcome
DeleteThanks so much
ReplyDelete